Mheshimiwa Rais Kikwete,

Kwa heshima na taadhima na mapenzi ya hali ya juu niliyonayo katika uongozi wako, siyo siri, ni dhahiri shahiri na kila mwana JF anaweza kuwa shahidi yangu kwa hilo.

Kikwete, nnaamini wewe ni mchapa kazi, nnaamini wewe una muono mpana na mrefu, nnaamini wewe unatimiza wajibu wako kwa kadri ya uwezo wako aliokujaalia Mwenyeezi Mungu.

Nakuomba yasikilize maneno ya William Lukuvi kwa umakini na ujifikirie, huyu William Lukuvi anaitakia mema Tanzania hii?

William Lukuvi amma kwa ujinga wake amma kwa werevu wake, ameutia dosari kubwa utawala wako. Ameenda Kanisani kuwaeleza Wakristo wenzake, tena kwa kujigamba na kejeli na kuonesha kibri ya hali ya juu, kuwa hana imani na Waislaam. Kumbuka iwe Muislaam wa Zanzibar au wa Tanganyika au kokote duniani, Waislaam ni kama kiwiliwili kimoja, unapokiumiza kidole kimoja basi mwili wote unasikia uchungu na unapatwa na maumivu.

William Lukuvi, yuko kwenye Serikali ambayo haina dini! lakini yeye mwenyewe ana dini na alienda kuongea kwenye nyumba ya dini na huko ndipo alipowaudhi Waislaam.

Hiyo ni dosari kubwa sana katika utawala wako. Tunakuomba muachishe kazi haraka sana William Lukuvi kabla hajazua balaa lingine, maana hata alipowahi kwenda kujitetea bungeni alionesha kibri zaidi ya kile alichoonesha Kanisani na akatamba na kuwachiwa muda na Mwenyekiti (mkristo pia) zaidi ya mbunge mwingi yeyote aliyechangia mijadala kwenye bunge maalum, ili ajitetee. Nilifikiri kuwa William Lukuvi ataomba radhi lakini cha kustaajabisha hajaomba radhi na karudia tena na tena na tena kuwa ana hofu na alichokieleza kanisani ni hofu yake na hakuna anaeweza kuhoji hilo.

Sisi tumemuelewa na hatumuhoji yeye, tunakuhoji wewe Rais wetu, jee, kiongozi wako ametugawa au ametuunganisha Watanzania kwa kauli zake hizo?

Jibu lako, mimi silijuwi, lakini jibu letu, ni wazi kabisa kuwa William Lukuvi katugawa Watanzania badala ya kutuunganisha, na si kuwa katugawa Watanganyika na Wazanzibari, la hasha, katugawa Waislaam na Wakristo. Na hilo ni hatari kubwa sana kwa Taifa letu.

Tunakuomba chukuwa hatua za haraka sana, umstaafishe huyu Waziri wako kabla hii athari na mpasuko alotuwekea kuzidi zaidi ya hapa alipotufikisha.

Msikilize:



Nnamalizia kwa kutoa shukrani zangu ikiwa utapata wasaa wa kuyaona haya niliyokueleza.