Friday 18 September 2015

Kambi Maarufu ya wahamiaji na wakimbizi, mjini Calais, nchini Ufaransa yenye kujulikana kwa jina la THE JUNGLE.


Hii ni Kambi ya Wahamiaji na Wakimbizi iliyopo Mjini Calais, Ufaransa.

Wengi wao ni kutoka Eritrea, Ethiopia, Libya, Afghanistan, Iran, Iraq, Sudan na Syria

"Kila aliyeko kwenye kambi hii mjini Calais si kwamba anapenda au anataka kuishi hapo Calais la hasha. Kila mtu aliyepo hapo ndoto yake ni kwenda kuishi nchini Uingereza."


Takriban watu 4,000 wanaishi katika kambi karibu na bandari ya mji wa Calais. Idadi kubwa ni vijana, lakini pia kuna wanawake wachache na watoto. Wengi wao ni kutoka Eritrea, Ethiopia, Libya, Afghanistan, Iran, Iraq, Sudan na wakimbizi kadhaa wanatoka nchini Syria.


Wote wamesafiri kwa muda wa wiki au miezi kadhaa au hata miaka wakizunguka nchi za Ulaya kwa lengo la kufika Calais, ambayo ipo maili zisizo pungua 30 kutoka mkondo wa bahari ya Waingereza kuelekea Uingereza (English Channel).

Hali ya kambi, si nzuri kabisa kwa binadamu yoyote kuishi humo.

Kambi imezungukwa na dampo, kiasi cha kusababisha matatizo ya kiafya kwa wakazi wake. Magonjwa kama vile ukurutu (Upele) ni jambo la kawaida – magonjwa yamacho na maambukizi ya kuumwa kifua unaosababishwa na vumbi na mchanga.


Na nje ya Kambi kuna uzio ambao una ncha kali na polisi wakipokezana ili kuwazuiya wale wote ambao watajaribu kuingia eneo ambalo magari makubwa yameegeshwa kusubiria zamu ya kuingia kwenye shimo au handaki ambalo linapita chini ya bahari kuanzia Ufaransa mpaka Nchini Uingereza.



Kuna mashirika yasiyopungua matatu na baadhi ya watu binafsi ambao wanajaribu kwa njia moja au nyingine kuwasaidia wahamiaji hao na wakimbizi waliopo hapo kambini.

Mara chache chache ukiwa ni mkaazi wa hapo unaweza kupata hema la kulalia, blanketi na hata vyakula vya kwenye makopo.


Wakazi wengi ambao wamejaribu kuingia Uingereza kwa kuruka uzio wa waya zenye ncha kazi wamejikuta wakijeruiwa aidha na waya zenye ncha kali au kupigwa na polisi wa ufaransa. Wapo ambao wamejikuta wakiumizwa na malori ya mizigo na hata kupoteza maisha.

Friday 11 September 2015

Waislam Tujihadhari na Kundi ili.

Miaka hii ya karibuni kumejitokeza baadhi ya watu, wakijitambulisha kwa mabandiko na picha mbalimbali za wapiganaji walioko uko Syria na Iraq, kwa jina maarufu ISIS.

Kwa mtazamo wa juu kwa juu, unaweza kuona kuwa watu hao wanapigania kuwepo na serikali ya Kiislam kwa maana ya khilafa na kabla ya hapo walijitangazia kuwepo kwa Majimbo ya Kiislam yaani Islamic State.

Kuna baadhi ya wanao jiita waislam kwa makusudi kabisa na kwa malengo yao maalumu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuwashawishi watu wawaunge mkono watu hawa. Na matokeo yake vijana wengi wameishia kukamatwa na vyombo vya usalama na kuozea jela.

Turudi nyuma kidogo na tutazame hawa wanao jiita Islamic state, wameanzaje na imekuwaje mpaka wamepata umaarufu kwa kipindi cha muda mfupi?
Mambo yote haya yemeanzia uko Iraq, baada ya serikali ya Sadam Hussein kuondolewa madarakani na kukaachwa kitu kinachoitwa Power vacuum (https://en.wikipedia.org/wiki/Power_vacuum), kwa maana ya kutokuwa na uongozi au waliokuwepo madarakani wanakuwa hawana uwezo wa kuongoza kiasi ya kujitokeza makundi makundi ambayo ujichukulia sheria na madara na kuongoza kwa namna wanavyo taka wao.

ISIS wameanza harakati zao mwaka 2006 katika moja ya vikundi vidogo vidogo ambavyo vilianzishwa kusaidia kusaka mabaki ya askari wa Sadam Hussein nchini Iraq. Kikiwa kikundi kidogo tu, kisicho kuwa na siraha za hatari kama walizonazo hivi sasa.

Ifahamike kwamba siku zote serikali ya Marekani, utafuta visingizio vya kushambulia nchi wanayotaka kuiba rasilimali zake au inapo ona kuwa kuna hatari ya kupoteza vyanzo vyake vya kiuchumi, na hapa kinacho zungumziwa ni Mafuta.

Nchi ya Marekani kuishambulia Syria moja kwa moja lingekuwa swala gumu na gharama zake zingekuwa na ukizingatia gharama walizo zitumia kwenye vita ya Iraq zilikuwa bado kurejeshwa. Na hapo hapo ndani ya Marekani hali ya kisiasa haikuwa nzuri kwa upande wa serikali iliyoko madarakani.
Ndipo wakaona kuyatumia makundi yalioko Syria, ili wawasaidia kuiondoa serikali iliyoko madarakani. Makundi haya yalionekana kuwa na misimamo tofauti na ile ambayo nchi za Kimagharibi zinataka, haya makundi yalitaka kuanzisha serikali ya Kislamu nchini Syria tu tofauti na ISIS, wao wakaja kuteka wazo na harakati zima zilizokuwepo na kujitangazia wao kuwa ndio wenye jukumu ilo.

Ndipo mwaka 2009 ISIS wakaitwa kwenda Syria ili kusaidia kumuondoa madarakani rais wa Syria Bashar Hafez al-Assad. Na lengo haswa halikuwa kumuondoa bali kuharibu harakati ambazo tayari zilikuwa zimeanzishwa vikundi vingine ambavyo vilisha anza kujipatia umaarufu kama vile Jabhat al-Nusra (al-Nusra Front) na Al-Jaysh (Free Syrian Army). Na hata ikitokea kundi au nchi yoyote ile kutangaza Khirafa basi ionekane kuwa utawala huo utakuwa ni wa kiuonevu na umwagaji wa damu. Kama vile tunavyo ona ISIS wakiwafanyia raiya wasi na hatia.

ISIS ndipo walipoanza kupata pesa na mafunzo rasmi ya mbinu za medani na ujanja wa kupigana mitaani kutoka kwa majeshi ya Amerika na washiriki wake kama Israel, Saudi, Jordan, Qatar, Uturuki, na Uingereza.

Rais Obama alipo hojiwa kuhusiana na kuviunga mkono vikundi vinavyoipinga serikali ya Bashar, alisema kuwa wanachowasaidia ni ushauri wa kiufundi na kutoa misaada ya kibinadamu tu. Kumbe kinyume chake walikuwa wakiwapatia pesa na siraha ambazo Marekani waliziacha Iraq, kama vile magari ya deraya, vifaru, mizinga ya kutungulia ndege na siraha nyingine nyingi.

Senate John McCain, alipo hojiwa alisema vita vya kuwapiga magaidi zinatarajiwa kudumu kwa miongo kadhaa, yaani si chini ya miaka thelathini.
Mwezi wa September 2013 habari zikaandikwa kwenye vyombo vya Kimarekani kuwa siraha ambazo USA kwa kutumia shirika lake la Kijasusi (CIA) wameweza kuwafikishia siraha na misaada mingine makundi yanayoipinga serikali ya Bashar, wakati huo huo kundi la Al-Jaysh (Free Syrian Army - FSA). Wakapinga kupata msaa wa siraha zozote kutoka serikali ya Marekani, japokuwa walikuwa wameahidiwa kupatiwa siraha. 



Wachunguzi wa habari za kimataifa wakajiuliza, siraha zimekwenda wapi, mbona makundi yaliokusudiwa yanalalamika kuwa hawakupata siraha. Serikali ya Marekani ikasisiza kuwa siraha zimekwisha wafikia walengwa. 

Haikuchukuwa muda mrefu ndipo mwezi Juni 2014 ISIS walipojitokeza wakiwa na siraha nzito uku wakiwa wamehitimu mafunzo ya kivita kutoka serikali ya Marekani na Israel. Na hata zilipotoka picha ambazo ISIS walipiga wakionyesha kuwa wameteka vifaru na siraha nyingine mbalimbali, nchi za Kimagharibi na haswa Marekani hawakuonyesha kushtuka, kwa sababu ilikuwa ni zawadi kutoka kwao.

ISIS ndio kundi tajiri la kipekee duniani, taarifa za kiuchunguzi zinasema kuwa licha ya misaada ya kifedha kutoka nchi zinazowaunga mkono, pia wanauza mafuta kwa kiwango kikubwa pato lake linakisiwa kwa siku kuwa ni zaidi ya dola za kimarekani milioni 1 kwa siku na fedha zingine zifikiazo dola milioni 20 zipatikano kwenye utekaji nyara na mapato mengine.


Marekani kwakutaka kujisafisha ikapiga baadhi ya visima vya mafuta na kuacha makampuni yenye kununua mafuta kutoka kwa ISIS yakiendelea kufanya biashara nao.

Wakati huo huo upande mwingine serikali ya Marekani inataka vita vya Syria viendelee muda mrefu, kwa sababu wanafaidia kwa upande mwingine, wanacho kifanya ni kuwapa pesa wapiganaji wa FSA ili vita iweze kuendelea muda mrefu, inakisiwa pesa walizopata ni dola za Kimarekani zipatazo milioni mia tano. Kundi ili alipewi siraha kama walizopewa ISIS kwa sababu watakapopewa siraha kuna uwezekano mkubwa wa ISIS kushindwa vita, kitu ambacho Marekani haitaki kitokee.


Waungaji Mkono

Wakati huohuo ili kundi liweze kupata kuungwa mkono na Waislam wasio jitambua au kuelewa kinacho endelea. Wameweza kulinasibisha kundi ili na Uislam na kuwa wanapigana Jihad kwa manufaa ya Uislam duniani. Hapo hapo wamesahau kuwa ISIS (Islamic State of Iraq and Syria) au ISIL (Islamic State of Iraq and the Levant) Neno Levant hapa linakusanya nchi Lebanon, Syria, na Israel. Wenyewe wanapigana kwa malengo mengine na uku wakijitambulisha kutaka kuzikomboa nchi zilizoko kwenye majina yao ambazo ni Iraq, Lebanon, Syria, na Israel.

Lakini ajabu utawakuta vijana wachache wasio jitambua, wanashinda kwenye mitandao ya kijamii, wakiwaunga mkono ISIS.

Haiwezekani kwa Muislam awe anauwa Waislam wenzake kisha ajitambe kuwa yeye ni Muislam, kisha watokee watu wawaunge mkono uku wakiwa na vijisimu vyao vya mkononi na wakijifanya kuwataka watu wakapigane upande wa Isis na Al-shabab.

Waislam wachache awa ambao wanatumiliwa na nchi za Kimagharibi ili kuonyesha kuwa wanapiga vita Ugaidi, lengo ni kuwaridhisha wananchi wao ambao ndio walipa kodi kuwa wanapiga vita ugaidi sin je ya nchi tu, hata ndani ya nchi zao.

Ndio ikaundwa program maalum ya kuwafundisha baadhi ya mashushu, ili kutafuta nani na nani wanaelekea kuwaunga mkono ISIS na magaidi wengine. Ndipo wakatengenezwa Waislam wasio jitambua au wenye kuendekeza matumbo yao, wakakesha mitandaoni na kujifanya kuwa wana uchungu sana na Uislam na wanawaunga mkono ISIS, ili hali wao wenyewe hata uwanja wa vita hawaujui unafananaje.

Mashushu awa uwa hawakamatwi, hata wakijitokeza hadharani na kuonyesha wazi kuunga mkono harakati za ISIS, Wanao kamatwa ni wale walioingia mkenge na kudhani kuwa wanakwenda kwenye JIhadi ya kweli kumbe ni kanyaboya. Wakisha wapata watu ambao wanaona kuwa wanawaunga mkono Alshabab au ISIS haraka sana wanawaripoti kwa mabwana zao na mara uishia jela.

Na hii ndio mbinu zinazotumika hivi sasa za kujifanya wanapambana na siasa kali (extremist) lakini kwa kuwa hakuna Uislam wa namna hiyo ndio kukawa na watu maalum kama hao ambao kazi yao ni kuangalia nani na nani wanaweza kuwashawishi. Wakisha wapata uweza hata kuwapa mafunzo na mbinu hafifu za hapa na pale, kisha kuwapatia tiketi za kugushi na kuwaelekeza waende viwanja vya ndege ili waende Syria. Lakini ghafla vijana hao ujikuta wapo mikononi mwa vyombo vya uslama na habari zao kuandikwa kwenye vyombo vya habari kuwa ni magaidi walikuwa wanakwenda Syria kusaidia ISIS au Alshab. Na raiya wan chi za ulaya wakiona hivyo uona kuwa serikali zao zinafanya kazi vyema za kuwalinda na magaidi wan je ya nchi na hata wa ndani ya nchi.

Hii inafanyika sana kwenye nchi za Uisngereza, Ufaransa na Marekani na nchi zile zinazopiga vita Uislam kivitendo.

Ukikutana nao vibaraka hawa wa kimagharibi, utasikia wakisema ISIS wanauwa Makafiri, Wanafiki na Washirikina, sasa tunawauliza. Kama mtume angeua Makafiri na washirikina wote wa Makkah sijui nani angebakia. Waislam waliokuja Afrika nao wangeua Makafiri na Washirikina wote walio wakuta, sijui mimi na wewe kama leo tungekua hapa, ni jambo lililo wazi kabisa babu wa babu zetu wangekuwa maiti na hata mimi na wewe tusingepata hata hii nafasi ya kuwa Waislam, maana ukiangalia wengi tunaweza kukuta Mababu zetu walisilimu kwa kuona tabia njema za hao walikuja na Uislam na ndio wakaupenda na kusilimu.

Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa makundi haya, utaweza kugundua kuwa makundi yote haya ni zao la Mmarekani na lengo ni kudhoofisha nchi zenye Waislam wengi ili wapate kuchukua wanacho kitaka kiurahisi.

Ndio tukaona uko Iraq walipoweza kuangusha serikali jambo la kwanza kufanya ni kulinda kwa nguvu zote vyanzo vyote vya mafuta. Na wkafanya hivyo hivyo nchini Libya.

Sasa wanasubiri Syria iangue rasmi kisha utaona wanapeleka majeshi kujifanya kuweka mambo sawa kumbe wanafata wanao yafata.



Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limemchagua Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Africa Dream mjini Dodoma, Wajumbe maalum wa BAKWATA imemchagua Sheikh Zubeiry kwa kura 310 za ndiyo baada ya kuingia kwenye uchaguzi huo akiwa mgombea pekee.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Alhaji Habib Ndassiwa alisema majina mawili yaliyotoka kwenye Baraza la Ulamaa yalikuwa ni ya Sheikh Ally Muhidini Mkoyogole na Sheikh Zubeiry.

Hata hivyo Sheikh Mkoyogole alijitoa na hivyo kumuacha Sheikh Zebeiry kuwa mgombea pekee.

Mufti Zubeiry aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya juu katika dini ya Kiislamu mnamo Juni 22 mwaka huu baada ya kifo cha Mufti Issa Shaaban Simba kilichotokea katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Alitakiwa kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (Siku Tisini) hadi Septemba mwaka huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi hiyo.

Monday 15 June 2015


Habari zilizotufikia muda si mrefu ni kwamba Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Issa Shabani Simba Amefariki dunia, leo asubuhi.

Mufti Shekh Issa Shabani Simba, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kisukari kwa muda mrefu kidogo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Mazishi ya Mufti Simba yatafanyika leo baada ya Swalat dhuhr shambani kwake uko Kigamboni.

Kwa wale wote watakaopata nafasi basi wanaweza kuudhuria Msibani nyumbani kwake Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

--DUA'A
Ewe Mwenyezi Mungu  hakika Issa Shabani Simba yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na adhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli, basi msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.

Wednesday 12 November 2014

By Kichaa Cha Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa

%^&*()+£€?# zenu....! Leo nahisi Kichaa changu kimepanda au sijui kimepandishwa, yaani hata sielewi, kinacho endelea vichwani mwa Wabongo wanaoishi ndani ya nchi ya Wachawi Giningi, heri mie Mwendawazimu Kichaa Aliyechanganyikiwa, kwa sababu hakuna anayeweza kuniangalia mara mbili, zaidi ya wale watoto wanaopenda kunitania na wengine wakifikiria kuwa eti nimesoma sana mpaka vitabu vikiniona vinachakaa vyenyewe, ndio akili zikaelewa saaaana mpaka nikawa Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa.

Hivi hawa wenye akili sana zilizopitiliza mpaka wakawa Wachawi, uwa wanafikiria nini kwenye vichwa vyao, hivi hawajui kuwa wale wenye akili robo ndio walio wachaguwa kuwa pale walipo? Eti nasikia kuwa baadhi ya vyama vya Kichawi vimeamua kuungana ili kukichangia na kukigomea chama Kikuu cha Wachawi.

Ah ah ah ah ah...! Kaaazi kweli kweli...! Wachawi awa awa si ndio kwenye Bunge lao la Wachawi, wamejipandishia masurufu kiasi cha kutisha, kama kweli hawa Wachawi wapo kule kutetea Misukule na Mandondocha, wangekuwa wanawashirikisha ndondocha na misukule wote kabla ya maamuzi yao. Lakini ni pale tu, Chama Kuu la Wachawi, likitumia uchawi wake mkuu, ndio utawaona Wanga na Wachawi wengine wakipiga kelele na kucheza mahepe, wakitaka kuwashirikisha ndondocha na misukule.

Nao Mandondocha na Misukule kwa kulewa na Uchawi na Urozi wa vyama vyao vya Kichawi wanawashabikia, wamelewa dawa za kuondoa akili a.k.a propaganda kiasi ya kwamba hawaoni hawasikii.  Ushabiki umekuwa mkubwa kiasi ya kwamba hawaoni wala hawasikii tena. Wanatamanishwa kila leo, lakini masikini hakuna wanacho kipata, wanaomba, wanatamani, mwisho tamaa na maombi yanasahaulika.

Wachawi wote, lao moja, sioni hata Mchawi mmoja mwenye afadhali. Sasa hivi kila kona unayokwenda Misukule na Mandondocha wanalalamika hali ngumu! Utamkuta mtu jicho limemtoka  kama yai la Mbuni "Hatukubali. Ngoja uchaguzi uje. Mchawi huyu sasa basi. Mimi kura yangu kwa naniu tu safari hii. Eeh, ndio! Mffvyyyy! Kshxnz$!!! kabisa! Blah...blah...blah...!"

 Ukiwa Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa kama mimi ndio unafaidi. Miye sina Mchawi hata mmoja ninaye mpenda. Usiniulize, kwa sababu Kichaa haulizwi, ukitaka kuwauliza bora uwaulize hao hao Misukule wenzio au waulize Mandondocha, ndio wenye uwezo, japokuwa hawajui kuwa wana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya maisha yao.

Nauliza tu wale wanaojidai wana hasira, hasira hizo ni za kweli au Vifuko vikitolewa tu, "Thalamaleku, uku wengine bwana athifiwe nyiiingi...!"

Wengi wanashangaa haswa lengo la haya ninayoyasema ni nini, wacha niwaambie kuwa sina lengo lolote, kwanza toka lini Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa akawa na malengo? Hayo malengo muwe nayo nyinyi wenye Akili na Wachawi wenu walio wafanya nyinyi kuwa Mandondocha na Misukule, mnalishwa pumba sawa! Mkilishwa Makapi sawa! Ila mkimwa matumbo, mkienda uko mnapo paita Sipiti-ni-hatari, I mean Sipatihali, Oops nina maanisha Hosipitali, ndio hosipitali, mnakumbana na maudhi mengine na kukatishana tamaa.

Hakuna Mafusho ya kufukisha wala, hirizi za kuwavika msiumwe magonjwa ya kuhara, matumbo yanasokota kwa kula pumba kavu, sasa unashangaa nini, kwani tangu lini, ndondocha au msukule akatibiwa?

Basi wacha niwaambie na nina uhakika kabisa Wandondocha na Misukule wote wamekwisha hukumiwa kifo tayari...! Ndio kwani hujui kuwa Bongoland, hukumu ya kifo inafanyakazi!?
Ndio inafanyakazi japokuwa si kwenye mahakama rasmi, lakini Wachawi wakishirikiana na Wanga wamesha wahukumu... Japokuwa si kile kifo cha kunyongwa hadi kufa kwa kuning'inizwa kambani au kupigwa risasi lakini cha moto wanakiona...! Maana wanakufa taratibu wakijiona na machozi yenda na maji hakuna wa kuyaona.

Tena siku hizi wachawi hawa wenye akili sana wamehamia Mbinguniiii kwa taarifa yenu. Maana hata kujenga wanajenga uko uko mbinguni, uku ardhini wanakuja tu, siku za Ijumaa na Jumapili, ili nao waonekane onekane, ili hali wanajuwa kuwa Mungu wao na Mungu wa Mandondocha ni tofauti.

Uko Sipiti-ni-hatari, I mean sipitali wanaotibiwa ni Wanga na Wachawi wenye kujiweza kidogo, kwa sababu, wao ndio Wabia wa nchi hii. Ila wale Manguli wa Uchawi walio na Ubia katika nchi hii... Unashangaa nini, ndio kwani hujui kuwa nnji hii imikwisha uzwa, shauri yako... Basi Wachawi wakipata faida, upeleka kuweka pesa zao uko mbinguni Uswisi. Wakitaka kufanya shopingi za wajukuu zao wanao wandaa kuja kutawala Ndondocha, wanakwenda zao mbinguni Dubai, mapumziko mbinguni Ufaransa, wakiumwa haoooo wenda zao mbingu ndogo India, ila Wachawi wengi wanaona kuwa mbingu ndogo India siku hizi hata baadhi ya Mandondocha wanakwenda, basi tena wamebadirisha, wenda zao Mbingu ya Londoni na wengini mbinguni Marikani.

Lakini ni ajabu sana Wachawi hawa, matibabu, shopingi, mapumziko yooooote yanafanyika Mbinguni, basi na mkifa Mzikwe uko uko Mbinguni, muwaambie jamaa zenu kabisaaaa, maana Bongoland sio Makaburini.

Ndioo... Eeeeh, Haiwezekani Mtumie mapesa yoote kwenye kujifaharisha uko Mbinguni, siku mkikata roho tu, mnaletwa duniani (Bongoland) kuja Kuzikwa, kwani mmesikia kuwa Bongoland ndio Makaburini, kwanini msizikwe uko uko Mbinguni kwenu!?
By Kichaa Cha Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa

Kwa wenye akili wengi wanaweza kushangaa na kichwa cha bandiko ili, watashangaa zaidi pale watakapo gundua kuwa mwandishi wake ni Mimi Mwendawazimu Kichaa aliyechanganyikiwa, Maana ukiwa na akili za Kichaa aliye changanyikiwa kama mimi, uoni tabu kuongea kile kilicho moyoni mwako kwa namna ambayo kichaa chako na uwendawazimu wako unavyo kutuma.

Kama wewe ni mmoja wapo wa wenye akili, usishangae na kichwa cha habari hapo juu, kwa sababu kimeandikwa na Kichaa Mwenye Wazimu.

Jambo moja unalotakiwa kufanya ni kutafakari kidogo ndipo utagundua kuwa neno baleghe lina maana ya kukomaa aidha kimwili (kibailojia) au kukomaa kiakili (intellectual) na hata kiroho (spiritual).

Kama ilivyo kuwa na umuhimu wa mwili kubaleghe kimwili (Kibailojia) vilevile kuna umuhimu kwa binadamu na haswa vijana Kubaleghe kiakili kwa sababu ni kitu muhimu sana katika kuleta mabadiliko ya kijamii. Vijana wengi tuna baleghe ya kimwili tu, huku tukikosa baleghe ya kiakili, na kiroho.

Ukosefu wa baleghe ya kiakili ni janga la kwanza kabisa kwa vijana wetu!

Kwa Kukosa baleghe ya Kiakili na Kiroho, ndiko kunako pelekea wengi wetu kukosa kuhishimiana katika majadiliano yetu na haswa tunapotumia mitandao ya kijamii.

Kuto kukomaa huku kunaletwa na kuzibemenda akili zetu na kuathili mioyo yetu kiasi cha kutoweza kuona thamani ya majadiliano yetu na kuhishimiana kwetu.

Tunacho angalia ni kuwa nimemshinda fulani, nimekuwa maarufu kwa kumtukana fulani au kwa kuwakufurisha watu fulani au kwa kuwashusha thamani kina fulani.

Tumeamua kwa makusudi kabisa kuzibemenda akili zetu na hatukubali mtu yoyote mwenye mawazo yanakwenda tofauti na yetu, kiasi cha kuwa vipofu wa akili kwa kushindwa kuona au kutambua kuwa binadamu tuna uwezo tofauti katika kuyakabili mambo mbalimbali katika jamii inayotuzunguka.

Wenye akili mnashindwa kuelewa kuwa, sisi WendaWazimu na Vichaa tulio changanyikiwa, ndio watu pekee ambao tunaruhusiwa kuto tumia akili zetu, kwa nyinyi mlio na akili kwa kuto tumia akili zenu ni kutunyang'anya haki yetu ya msingi kwa sababu sisi ni vichaa na zaidi ya hapo tumechanganyikiwa.

Ajabu ya nyinyi ambao mna akili, hamtukubali tena kujifunza kutoka kwa wenzenu wenye akili kama nyinyi au wenye mitazamo tofauti na yenu, hamzisomi tena hoja zao, hata kama zina ukweli au hazina ukweli. Mnacho kiangalia ni kile ambacho mnakiona kuwa ni sawakwa akili zenu na hata kama si sawa mnakibeba tu hivyo hivyo kama kilivyo, hamjali tena, mnacho kijali ni kitu kimoja tu, kuwa maarufu hata kwa kupinga ukweli ambao kila kukicha mnaukimbia.

Siku mtakapokubali kuwasikilia wale mnao waona kuwa ni maasimu wenu, ndipo mtakapo gundua kuwa wale ambao mkiwaona kuwa ni maasimu wetu kumbe ni ndugu, jamaa na marafiki zenu na wanacho kieleza aidha kina manufaa na ukweli ndani yake au tofauti yenu ni ndogo sana na si tofauti ya kuwafanya muwachukie na kuwaona kuwa ni maadui zenu.

Ikiwa kwa sababu ya upuuzi wenu hamutaweza kuona sura zenu hasa katika kioo cha vitendo vyenu, mtakuwa mmefanya kosa kubwa lisilosameheka. Kabla ya lolote lile, ni wajibu kwenu kwanza kuzichungua hali zenu za kiroho na kuziona waziwazi sura zenu za ndani, ili mweze kuzitambua aibu zilizoota mizizi na kustawi katika dhamiri zenu bila ya nyinyi wenyewe kufahamu.

No nyinyi wenyewe ndio mnaoweza kuikata mizizi ya sifa mbaya katika nafsi zenu kwa kufanya uchunguzi na jitihada, na kuzizuia (nafsi) zisidhihirishe ubaya wake katika mazingira ya maisha yenu.

Hakika mmeshafanya makosa na mnaendelea kufanya makosa, mnajitenga na tabia za Kiislam na mnatufundisha sisi wendawazimu mambo mabaya na hata kwa vizazi vyetu na vyenu nyie wenye akili kwa maana ya watoto zetu sote.

Hakika tunakitenga kizazi na dini yetu. Hawakukosea wale waliosema: "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo."

Na kwa kweli wanatusoma kwa haya tunayo yaandika kwenye mitandao.

NB:
Usiniulize, kwa sababu Kichaa Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa, hawezi kujibu maswali ya Wenye Akili kama wewe.

Alamsiki

Assalamu Alaikum Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh

Kwenye jamii zetu, kuna maradhi mbalimbali yanayosumbua siha zetu, kuna huu ugonjwa ambao sina jina rasmi la kuupa, lakini unashambulia sana bongo zetu haswa sisi Waislam.

Ugonjwa huu wa akili uja katika hali tofauti tofauti kulingana na mweuko wa muhusika mwenyewe. Kuna ambao wapo kwenye mashindano ya kifikra, hapa ndipo inazaliwa hali ya watu kutaka kujikweza. Kukosa au kukataa fikra zao kunakuwa kama ni fedheha, na wanakuweka kwenye kundi la ufai na kwanini huwi kama wao.

Maana katika ugonjwa huu ambao uwapata wale wenye akili usababisha kujikweza, kujiona bora zaidi kuliko wengine, na kwamba wao ndio wanaostahili kusema, kukejeri, kutukana wengine, na kila mwenye kukataa fikra zao basi huyo ni mwenye kushutumiwa na hafai katika jamii ya wenye Akili kama wao. Wenye akili awa upelekea mpaka watu kujiona kuwa pepo ya Mwenyezi Mungu ni yao na funguo za pepo zote wamekabidhiwa wao. Na wao ndio wanaostahili kuwa mabwana, na wengine wote wawe watwana. Kiasi cha kujuwa nani wa kumuingiza peponi na nani wa kumwingiza motoni.

Kuna makundi katika iymaan ya Kiislam, haya makundi yalishatabiliwa uwepo wake, na haya makundi ni katika jitahada za hao walikuwepo nyuma katika kufutu maswala ya kiiymaan na katika fiqh, tatizo linakuja kwa hao wafuasi wa hayo makundi, badala ya kufuata mwenendo mwema wa hao wanao wafuata, wao wamejikuta wanaathirika na huu ugojwa wa kuwa na akili nyingi wenye kushambulia milango ya ufahamu na kiasi cha kutokuwa na hikam wala busara za kimazungumzo, Akili zao upanda na kujiona wao ni malaika  kiasi kumfanya mwelevu huyu kujikweza na kujiona kuwa ana haki ya kila jambo na kuwapa watu kile ambacho yeye anaona kinastahili kwa muda ule.

Mara nyingi maulamaa awa wenye akili uwa wanashadidia mambo kiasi cha kujisahahu kuwa wao ni Waislam na hao wanaowashadidia ni Waislam na wanastaili hishma na staa kama wanavyo stahiki wao.

Jamii hii yenye akili huwa ina maradhi ya kiakili yaitwayo Prejudice, maradhi ya kuwaona wengine si kitu katika lolote lile na kuwa na chuki bila sababu, wakati mwingine fikra zao uwapelekea kuwaona makafiri ni bora kuliko yule anayepingana na hayo maradhi ya akili... Na hata wakileta jambo la uwongo basi hapana mtu yoyote anayestahiri kulikosoa, maana katika akili zao na maradhi walionayo wanajiona kuwa wao ndio mwisho wa fikra na hakuna ambaye anastahili kukosoa au kuzungumza kuhusiana na jambo walilolileta. Na hawastahili hishma wala hadhi kama walio nayo wao...!

Wenye akili awa wamefanikiwa sana katika kueneza chuki miongoni mwa jamii za Kiislam kiasi cha kuwafanya wawe mbilikimo wa kifikra (intellectual dwarf), wamefanikiwa kuwagawa Waislam katika makundi, kiasi ya kukosa tena ule upendo wa Kiislam katika jamii, ukiwa ukubaliani nao basi wewe ni msaliti, aidha ukubali kujinasibisha na moja ya makundi yao au ukubali wakutusi na kukukejeri na kukuita majina yote mabaya wanayo yajuwa wao.

Wamekuwa vipofu kiasi ya kwamba wanashindwa kusoma hata ayah za Qur'an...!

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.
Qur'an Surat Al I'mran 103

---
By Kichaa Mwendawazimu Aliyechanganyikiwa

99Graphix

99Graphix
99Graphix
Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!