Friday 11 September 2015


Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limemchagua Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Africa Dream mjini Dodoma, Wajumbe maalum wa BAKWATA imemchagua Sheikh Zubeiry kwa kura 310 za ndiyo baada ya kuingia kwenye uchaguzi huo akiwa mgombea pekee.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Alhaji Habib Ndassiwa alisema majina mawili yaliyotoka kwenye Baraza la Ulamaa yalikuwa ni ya Sheikh Ally Muhidini Mkoyogole na Sheikh Zubeiry.

Hata hivyo Sheikh Mkoyogole alijitoa na hivyo kumuacha Sheikh Zebeiry kuwa mgombea pekee.

Mufti Zubeiry aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya juu katika dini ya Kiislamu mnamo Juni 22 mwaka huu baada ya kifo cha Mufti Issa Shaaban Simba kilichotokea katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Alitakiwa kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (Siku Tisini) hadi Septemba mwaka huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

99Graphix

99Graphix
99Graphix
Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!