Polisi
wa Tanzania walivunja zoezi la mafunzo ya al-Shabaab katika mkoa wa
Tanga, kuwakamata washukiwa 69 na kuwaachia huru dazani za wafundishwaji
wakiwa na umri wa miaka kati ya 4 hadi 13 katika usafishaji wa usalama
uliofanyika tarehe 28 Oktoba hadi tarehe 5 Novemba.
"Hii
imetushitua, tumeongeza usalama katika wilaya ya Kilindi na
tumewasambaza polisi jamii wa kutosha ambao wanalijua eneo vizuri, na
kupitia operesheni za pamoja na polisi wetu tunapaa majibu yanayotia
moyo," Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga Constantine Massawe aliiambia
Sabahi, akihakikisha idadi ya waliokamatwa.
Siku
ya kwanza ya operesheni, polisi waliwaachia watoto 54 na wanawake 32
ambao walikutwa katika kituo cha mafunzo huko Lwande na kuwaunganisha
tena na familia zao katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, kwa mujibu
wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa.
Kuzitia kasumba akili changa
Watoto
wengine 20, wenye umri wa miaka kati ya 4 na 13 na ambao "wamefundishwa
kikamilifu" na al-Shabaab katika msikiti wa wenyeji, walikuwa wamewekwa
katika programu ya urekebishwaji, Liwowa aliiambia Sabahi.
Wakati
polisi walipowakuta katika msikiti wa Madina, vijana hao walikuwa na
madaftari yaliyokuwa na mafunzo ya "jinsi ya kuua kwa kutumia kisu [au]
panga, jinsi ya kupambana na wabishi kwa kutumia silaha na bila
[silaha], jinsi ya kuhujumu uchumi na jinsi ya kuikomboa Afrika
Mashariki katika mikono ya makafiri [infidels]," kwa mujibu wa Liwowa.
Al-Shabaab
waliwafundisha watoto hawa katika kiwango kwamba walijitoa kwa wazazi
wao kama sio Waislamu wa Kweli kwa sababu wanashirikiana na wasiokuwa
Waislamu, alisema.
Wakati
wa msako katika msikiti huo, polisi pia walikamata mikanda ya video 12
yenye mafunzo ya al-Shabaab ya jinsi ya kuwakomboa Waislamu Afrika
Mashariki na dunia kwa ujumla, alisema.
Kiongozi
wa kikundi, mwenye jina la Ayubu na anayejulikana kama "Master",
alikimbia dakika chache kabla ya kuwasili kwa polisi msikitini, lakini
walimkamata msaidizi wake, mkaazi wa mkoa wa Singida aliyebainishwa kama
Bw. Jumanne, alisema Liwowa.
Watoto
walikabidhiwa kwa wafanyakazi wa kijamii kwa ajilii ya programu ya
mabadiliko ya wiki tatu, alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego.
Kama wako tayari, watoto wataunganishwa tena na familia zao, alisema.
"Mshangao
wangu ni jinsi watoto hawa wadogo wavyolikuja kukutana na wafundishaji
hawa," Dendego aliiambia Sabahi. "Unamkuta mtoto wa miaka minne ambaye
wazazi wake hawajulikani, na unashangaa ni jinsi gani walimshikilia
mtoto mdogo kama huyu."
Wazazi
wanahitaji kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto wao shule
ili wasiangukie katika makundi ya kigaidi, alisema Dendego.
Kuongezeka kwa vitisho vya al-Shabaab?
Kuwepo
kwa al-Shabaab wilayani humo kulitambulika ndani ya wiki ya mwisho ya
mwezi Oktoba, wakati wananchi wasamaria wema walipowafahamisha viongozi
wa serikali kuhusu kambi ya mafunzo iliyopo katika msitu wa Lwande.
"Tulipata
taarifa kutoka kwa wasamalia wema, hususan wafugaji ambao mifugo yao
ilikamatwa kila ilipokatiza jirani na kamba hiyo ya mafunzo," alisema
Liwowa. "Pia, [wafundishaji wa al-Shabaab] walikuwa wakiwafukuza na
kuwanyang'anya ardhi wenyeji kwa kiasi ambacho walipata ekari 500."
Viongozi
wenyeji wamejifunza kwamba wafundishaji wanne wa al-Shabaab waliwasili
katika wilaya ya Kilindi mwaka 2008 na kujiunga na msikiti wa Madina,
lakini wanakijiji walijitenga na wafundishaji baada ya kuona mawazo yao
yalikuwa na msimamo mkali, alisema Liwowa.
"Baada
ya mapigano hayo mwishoni mwa mwaka 2008," yakitokana na mzozo
uliotokea ndani ya msikiti kati ya wenyeji na wanachama wa al-Shabaab,
"wafundishaji hao walinunua kipande chao cha ardhi na kujenga msikiti
tofauti ambao sasa waliutumia kufundishia mafunzo ya al-Shabaab,"
alisema.
Kutokana
na taarifa zilizokusanywa hadi sasa, baadhi ya watoto waliopata mafunzo
kutoka kwa al-Shabaab katika wilaya ya Kilindi wamepelekwa Somalia
kupitia Mombasa, Kenya, alisema Liwowa. Idadi kubwa ya wafundishaji wa
al-Shabaab kutoka Somalia na Mombasa pia walikuja Kilindi mwanzoni mwa
mwaka 2013, na inaonekana kuwa na mkakati wa ufundishaji katika mikoa
mingine, kama vile Kilimanjaro, Zanzibar, Pwani na Mtwara.
Operesheni ya polisi katika wilaya ya Kilindi inafuatia ukamatwaji wa tarehe 7 Oktoba wa washukiwa 11 wa al-Shabaab waliokuwa wakifanya mafunzo ya kijeshi katika mkoa wa Mtwara.
Aidha, polisi walimkamata mfanyabiashara wa Tanzania Juma Abdallah Kheri tarehe
31 Oktoba huko Tanga kwa kushukiwa kwamba alikuwa akijihusisha na
kuwaghiramia makundi ya kigaidi nchini Tanzania na washirika wa
al-Shabaab nchini Kenya, Kituo cha Vijana Waislamu.
Alipoulizwa Tanzania inafanya nini kukabiliana na vitisho vya al-Shabaab vinavyoonekana kuongezeka,Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosaya Jinai Robert Manumba alisema polisi walikuwa wakishirikiana na mashirika mengine ya usalama kupamaba na tatizo hilo.
"Tumeunganisha
idara zote za usalama kuunda timu maalumu. Timu hiyo inahusisha maofisa
usalama kutoka polisi, jeshi, huduma yetu ya upelelezi ya taifa,
uhamiaji na [Mamlaka ya Mapato Tanzania] ambao wanafanya kazi kwa
kushirikiana kutafuta suluhisho litakalodumu," Manumba aliiambia Sabahi.
0 comments:
Post a Comment